Ms. Belinda shares her insightful experience of our community outreach activity. Towards the end of 2023, she spent three weeks alongside two colleagues in Nsimbo leading an awareness campaign in 18 villages of Nsimbo District Council, north of Katavi National Park. This area is surrounded by numerous conserved areas, ranging from community forest reserves, national forest reserves, game reserves, and national parks which host a significant number of wildlife populations. Nsimbo experiences high incidences of human-wildlife conflict and qualifies to be among our priority areas for conservation education and outreach. Please click this link to read the full article.
Ecological Study Trips with Students
Hello everyone, here is yet another exciting article from one of our committed staff highlighting students’ outdoor learning activities through field visits. It was launched in 2023 with the initial support of Nomad Tanzania but it turned out to be the most liked student activity amongst the youth program. Please open this link to access the article.
umuhimu wa tembo katika mazingira, uchumi na utamaduni
Tembo ni mnyama wa nchi kavu jamii ya mamalia. Ndiye mnyama mkubwa kuliko wote waishio nchi kavu. Kuna aina mbili za tembo duniani, tembo wa bara la Afrika na tembo wa bara la Asia. Kuna spishi mbili za tembo wa Afrika; tembo wa msituni na tembo wa uoto wa savana. Tanzania ina tembo wa savana pekee. Tembo wa msituni hupatikana katika nchi za Afrika ya Kati na Magharibi.
Tembo anakadiriwa kuwa na uzito wa kilo 6600 (tani 6.6) kwa madume na kilo 3300 (tani 3.3) kwa majike. Tembo huishi miaka 60 hadi 70. Tembo hupendelea kula mimea, magome ya miti, matunda,majani na nyasi. Kuna tofauti kati ya tembo dume na tembo jike. Tembo dume huwa na mwili mkubwa uliojengeka, paji la uso huwa na mviringo lakini tembo jike huwa na paji lililochongoka.
Faida za tembo kiuchumi;
Hapa nchini, kwa zaidi ya asilimia 90 ya utalii unategemea wanyamapori. Watalii wengi huja kuwaona wanyama, kuwapiga picha na kuondoka. Wanyamapori wamebeba utalii kwa kiasi kikubwa na utalii umesaidia kukuza uchumi wa nchi hii – Wanyama hawa kupitia utalii wanasaidia kupata fedha za dawa, vitabu mashuleni, wanatujengea barabarana miundo mbinu nyingine na pia wanalipa mishahara kwa watumishi wa umma.
Huchangia patika pato la taifa. Tembo pamoja na wanyamapori wengine wamekua kivutio kikubwa cha utalii hivyo hutusaidia kupata hata fedha za kigeni ambazo husaidia maendeleo ya kiuchumi ya nchi yetu. Mfano sekta ya utalii kwa mwaka 2016 ilichangia 17.5% ya pato la taifa na 25% ya fedha za kigeni.
Chanzo cha ajira. Uwepo wa tembo na wanyama wengine umepelekea watu wengi kuajiriwa katika sekta ya wanyamapori na utalii. Kwa mfano mwaka 2016, watu takriban 600,000 waliajiriwa moja kwa moja katika sekta ya utalii na wengine takriban milioni moja katika ajira mbadala.
Ni kivutio cha watalii. Tembo ni mnyama ambaye ana mvuto sana kutokana na ukubwa, uzuri wake wa asili na muundo wa jamii na tabia yake. Takwimu za mwaka 2016 zinaonyesha kuwa watalii waliotembelea Tanzania walikua 1.284,279 ambao ni ongezeko la 12.9% ukilinganisha na mwaka 2015 ambao watalii waliofika Tanzania walikua milioni 1,137,182.
Faida Za tembo kitamaduni:
Tembo ni urithi wa Taifa letu. Tembo ana umuhimu sana katika utamaduni wa kiafrika. Kwa mfano, hutokea katika mapambo kama vile hereni, pete na hata michoro ya kwenye mavazi. Pia tembo wana nafasi maalumu katika hadithi za kiafrika. Hivyo tembo, kama wanyama wengine ni urithi wa taifa letu.
Faida za tembo kimazingira.
Tembo ni mnyama tegemeo kwa wanyama wengine na muhimili mkubwa katika mfumo wa ikolojia. Mfano, wakati wa kiangazi tembo hutumia meno yao kuchimba maji ardhini, hii huwawezesha tembo kuishi katika mazingira kame. Maji hayo huwafaidisha wanyama wengine wakubwa na wadogo. Pia wakati wa kiangazi tembo huangusha matawi makubwa ya miti ambayo huwawezesha wanyama wadogo kupata chakula mfano swala, pundamilia na hebivora wengine.
Tembo husaidia kusafisha na kutengeneza mazingira ya mbuga. Tembo wasingekuepo, mazingira ya savana yangeonekana tofauti sana. Tembo hula mimea na vichaka vya miti ambapo hufungua misitu na mapori kuwa mbuga wazi kutoa nafasi kwa mimea mengine kuota na njia kwa wanyama wengine.
Tembo husaidia kuongezeka kwa idadi ya mimea. Hii ni kutokana na ulaji wao wa mimea yenye mchanganyiko wa mbegu mbalimbali. Popote wanapoishi huacha kinyesi kilichojaa mbegu. Mbegu hizi huchipua na kuwa nyasi, miti na hata misitu hivyo husaidia kuongezeka kwa mimea na afya ya mazingira kwa ujumla.
Kinyesi cha tembo ni chanzo cha chakula kwa wanyama kama tumbili, ndege na nyani. Pia kuna wadudu hutegemea kinyesi cha tembo kama chakula mfano mende kibyongo (dung beetle). Kinyesi cha tembo pia ni chanzo cha rutuba katika udongo hivyo kuongeza afya ya mazingira.
Pamoja na faida nyingi za tembo, kuna changamoto nyingi zinazomkabili mnyama huyu mfano ujangili na migogoro baina yao na binadamu. Ujangili umeongezeka kutokana na uwepo wa biashara ya meno ya tembo katika masoko ya bara la Asia. Serikali inapaswa kuunga mkono jitihada za kimataifa za kuikakabili biashara hii kwani kuna mataifa tayari wameshaonyesha nia ya kufunga masoko kwa mfano China.
Jukumu la kuzuia ujangili si la serikali pekee. Dhana hii ni potofu kabisa kwani, uzuiaji ujangili kamwe hautafanikiwa kama wananchi na wadau wengine walioko ndani na nje ya nchi yetu wataendelea kubakia watazamaji tu. Ni muhimu kila mwananchi mzalendo wa nchi hii ashiriki kikamilifu katika ulinzi wa nchi na rasilimali zake zote kama katiba ya nchi inavyotuasa.
Elimu kuhusu shoroba za tembo na mienendo ya tembo inafaa kutolewa kwa watu waishio pembezoni mwa maeneo ya hifadhi. Hii itapunguza shughuli za binadamu katika maeneo hayo hivyo kuepusha migogoro hii.
Wanyamapori, tembo wakiwemo kama ilivyo kwa viumbe hai, huzaliana. Hivyo, kama tutashirikiana kuwalinda na kuwatumia kiendelevu si miaka mingi tangu sasa watakuwa namba moja katika kuchangia pato la Taifa letu.
Makala haya yameandaliwa na wanafunzi kutoka shule ya upili Usevya kwa kushirikiana na mradi wa Vijana na Mazingira